Soma Biblia Kila Siku 11/2020预览

Yohana alipozama katika uwepo wa Mungu aliona mengi yahusuyo ufalme wa mbinguni. Alionyeshwa picha ya mambo yaliyopo, na aliwaona watu wengi wakimsifu Mungu wakifurahia wokovu wake. Je, una hamu ya kufika hapo? Ila unajiuliza una uhakika gani? Ukizama katika Neno la Mungu, yeye atakuonyesha jibu sahihi. Tafakari tena m.3 unaosema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.Zingatia Mungu anavyotawala vitu vyote. Endelea kumtegemea yeye, naye atakulinda mpaka utakaporithi uzima wa milele pamoja na ule mkutano mkubwa. Maana wokovu una Mungu!
读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More