Soma Biblia Kila Siku 07/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

31天中的第9天

Yesu alitembea juu ya maji. Hata Ulaya watu hutembea juu ya maji. Lakini watu hawalihesabu kama mwujiza, maana wakati wa baridi maji yanaganda na kugeuka kuwa magumu kama kioo. Ikiwa ni baridi sana, hata magari hupita juu yake! Ila katika nchi za joto kama Tanzania au Israeli maji hayagandi, na mtu hawezi kutembea juu yake bila kuzama. Kwa Yesu iliwezekana kwa sababu ni Mwana wa Mungu. Zingatia wanafunzi wake walivyosema na kufanya: Waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu(m.33)! Vyotevilifanyika kwa huyo (hata maji!); wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika (Yn 1:3).

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More