Soma Biblia Kila Siku 8预览

Aya za 14-17 na 19 zabeba maudhui ya 2 Kor 6:14-18, Msifungiwe nira pamoja na wasioamini. Ubaya wa dhambi una sifa ya kuunyonya uzuri ndani ya wanadamu. Licha ya kupoteza njia ya Mungu, hata wangelewa uovu (m.16-17). Kwa hiyo ni hatari kwa mtu yeyote kushirikiana na watu waovu. Tunatakiwa tuwapende, kuwahurumia na kuwaonyesha njia, lakini tujitenge dhahiri na matendo yao. Tufanyeje? Linda moyo wakokwa uangalifu wote, ukihifadhi neno la Mungu ndani yake, maana ndiko zitokazo chemchemi za uzima(m.23). Hivyo utakuwa nuru.