2 Wafalme UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha pili cha Wafalme ndicho kinachofuata kitabu cha kwanza kuhusu mfululizo wa habari tunazopewa. Humu tunapewa habari za utawala wa wafalme wa mwisho wa Israeli na Yuda.
Sehemu ya kwanza ya kitabu hiki (sura 1-17) yahusu habari za Ahazia, mfalme wa Israeli mpaka wakati wa kuangamizwa kwa utawala wa Kaskazini wa Israeli kulikosababishwa na upotovu wa uaminifu kwa Mungu kwa upande wa wafalme wake. Kutokana na ukaidi wa wafalme hao Mungu alimruhusu mfalme wa Ashuru, Shalmanasari, kuuvamia Samaria, mji mkuu wa utawala huo wa kaskazini, mnamo mwaka 722 K.K. na kuchukuliwa uhamishoni wengi wa wakazi wake. Sura nyingi za sehemu hii zinatupatia habari za nabii Elisha ambaye alishika nafasi ya Elia (sura 2-23).
Sehemu ya pili ya kitabu hiki, yaani sura 18-25, inahusu visa vya miaka 130 ambavyo viliukumba utawala wa kusini, yaani Yuda, mpaka wakati Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, alipouvamia mji wa Yerusalemu mnamo mwaka 587 K.K., akaliharibu hekalu na kuwachukua wengi wa watu mashuhuri wa Yuda mpaka Babuloni (sura 25). Maafa hayo yaliyoukumba utawala wa kusini wa Yuda na yale yaliyoupata utawala wa Kaskazini wa Israeli, yanaelezwa kuwa matokeo ya ukosefu wa imani kwa Mungu.

高亮显示

分享

复制

None

想要在所有设备上保存你的高亮显示吗? 注册或登录