1
Mwanzo 25:23
Neno
NEN
BWANA akamjibu, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na mataifa hayo mawili kutoka ndani yako watatenganishwa. Mmoja atakuwa na nguvu kuliko mwingine, na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”
موازنہ
تلاش Mwanzo 25:23
2
Mwanzo 25:30
Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)
تلاش Mwanzo 25:30
3
Mwanzo 25:21
Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. BWANA akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.
تلاش Mwanzo 25:21
4
Mwanzo 25:32-33
Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?” Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
تلاش Mwanzo 25:32-33
5
Mwanzo 25:26
Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini Rebeka alipowazaa.
تلاش Mwanzo 25:26
6
Mwanzo 25:28
Isaka, aliyekuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.
تلاش Mwanzo 25:28