Zaburi 129

129
Maombi juu ya waadui za Israeli
1Wimbo wa safari za kidini.
Kila mutu katika Israeli aseme:
“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu”.
2Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu,
lakini hawakunishinda.
3Walinikata vidonda katika mugongo,
kama wanavyolima matuta katika shamba.
4Lakini Yawe ni mwenye haki;
ametutosha katika utumwa wa hao waovu.
5Wafezeheke na kurudishwa nyuma,
wote wale wanaouchukia Sayuni.
6Wakuwe kama nyasi juu ya paa la nyumba,
ambazo zinanyauka mbele ya kukomaa,
7anayezikata hajazi kitanga cha mukono,
wala anayezikusanya haenezi fungu.
8Naye anayepita karibu asiwaambie:
“Yawe awabariki!
Tunawabariki kwa jina la Yawe!”

Seçili Olanlar:

Zaburi 129: SWC02

Vurgu

Kopyala

Karşılaştır

Paylaş

None

Önemli anlarınızın tüm cihazlarınıza kaydedilmesini mi istiyorsunuz? Kayıt olun ya da giriş yapın