Zaburi 121

121
Mungu ni mulinzi wetu
1Wimbo wa safari za kidini.
Ninainua macho kwenye milima.
Musaada wangu unatoka wapi?
2Musaada wangu unatoka kwa Yawe,
aliyeumba mbingu na dunia.
3Hatakuacha uanguke;
mulinzi wako hasinzii.
4Kweli mulinzi wa Israeli
hasinzii wala halali.
5Yawe ni mulinzi wako;
yuko upande wako wa kuume kwa kukukinga.
6Muchana jua halitakuchoma,
wala mwezi hautakuzuru usiku.
7Yawe atakukinga na uovu wote;
atayalinda salama maisha yako.
8Yawe atakulinda katika shuguli zako zote#121.8 katika shuguli zako zote: Kiebrania: unapoingia na kutoka.
tangu sasa na hata milele.

Seçili Olanlar:

Zaburi 121: SWC02

Vurgu

Kopyala

Karşılaştır

Paylaş

None

Önemli anlarınızın tüm cihazlarınıza kaydedilmesini mi istiyorsunuz? Kayıt olun ya da giriş yapın