Yohana 1
NEN
1
Neno Alifanyika Mwili
1 # 1Yn 1:2; Yn 17:5; Flp 2:6; Isa 55:11 Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2#Ufu 1:8; Mwa 1:1Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
3 # Kol 1:16; Ebr 1:2 Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4#1Yn 5:20; Ufu 1:8; Yn 12:46Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5#Yn 3:19Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda.
6 # Mt 3:1 Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7#Yn 3:26; 5:33; 3:15Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini. 8#Yn 1:20Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 9#1Yn 2:8; Isa 49:6Kwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni.
10 # Yn 1:3; Ebr 1:2; 11; 3 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. 11#Lk 19:14; Mdo 3:26; 13:46Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 12#Isa 56:5; Rum 8:15; Gal 3:26; 2Pet 1:4; 1Yn 3:1Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13#Tit 3:5; Yak 1:18Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
14 # 1Yn 1:1-2; 4:2; Yn 14:6 Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
15 # Yn 1:32; 3:32; 5:33; Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:27, 30; 3:31; 8:58; Kol 1:17 Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ” 16#Kol 1:19; 2:9Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17#Kum 32:46Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.
Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji
(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)
19 # Yn 7:1; 10:24 Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20#Yn 3:28; Lk 3:15-16Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”#1:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
21 # Kum 18:15; Mt 11:4 Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”
Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”
“Je, wewe ni yule Nabii?”
Akajibu, “Hapana.”
22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”
23 # Mt 3:1; Isa 40:3 Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”
24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25#Mt 21:25wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”
26 # Mt 3:11; Mk 1:7, 8 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,#1:26 Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji. lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 27#Yn 3:26; Mdo 13:25Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”
28 # Yn 3:26; 10:40 Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.
Yesu Mwana-Kondoo Wa Mungu
29 # Mwa 22:8; Ufu 5:6 Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30#Yn 15:27Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 31#Mal 3:1; Mt 3:6; Lk 1:17, 76, 77; 3:3, 4Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”
32 # Mt 3:16; Mk 1:10 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33#Mk 1:4; Mt 3:11Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34#Mt 4:3Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”
Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu
35 # Mt 3:1 Siku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36#Yn 1:29Alipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!”
37Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38#Mt 23:7Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”
Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?”
39Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”
Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.
40 # Mt 4:18-22 Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu. 41#Yn 4:25Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 42#Mwa 32:28; Mt 16:18Naye akamleta kwa Yesu.
Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro#1:42 Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake ni Kipande cha mwamba.).
Yesu Awaita Filipo Na Nathanaeli
43 # Mt 10:3; Yn 14:8-9; Mt 4:9 Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”
44 # Yn 12:21 Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 45#Yn 21:2; Lk 24:27; Mt 2:23; Lk 3:23Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.”
46 # Yn 7:41-42, 52 Nathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”
47 # Za 32:2; Rum 9:4-6 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hana hila ndani yake.”
48Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?”
Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”
49 # Mt 23:7; 4:3; 2; 2; 27:42 Nathanaeli akamwambia, “Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”
50Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 51#Mt 3:16; 8:20; Mwa 28:12Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Узнать больше о Neno: Bibilia Takatifu 2014