Zaburi 58
58
Zaburi 58
Mungu kuwaadhibu waovu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi.
1Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki?
Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu?
2 La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu,
na mikono yenu hueneza jeuri duniani.
3 Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,
toka tumboni mwa mama zao
ni wakaidi na husema uongo.
4 Sumu yao ni kama sumu ya nyoka,
kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,
5 ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi,
hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani.
6 Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao;
Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba!
7 Na watoweke kama maji yanavyotiririka;
wanapovuta pinde zao, mishale yao na iwe butu.
8 Na wawe kama konokono anayeyeyuka akitembea,
kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu.
9 Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba,
zikiwa mbichi au kavu,
waovu watakuwa
wamefagiliwa mbali.
10 Wenye haki watafurahi wakilipizwa kisasi,
watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu.
11 Ndipo wanadamu watasema,
“Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu,
hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.”
Selectat acum:
Zaburi 58: NEN
Evidențiere
Copiază
Compară
Împărtășește
Dorești să ai evidențierile salvate pe toate dispozitivele? Înscrie-te sau conectează-te
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.