Zaburi 132
132
Zaburi 132
Maskani ya Mungu ya milele huko Sayuni
Wimbo wa kwenda juu.
1Ee Bwana, mkumbuke Daudi
na taabu zote alizozistahimili.
2 Aliapa kiapo kwa Bwana
na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3 “Sitaingia nyumbani mwangu
au kwenda kitandani mwangu:
4 sitaruhusu usingizi katika macho yangu,
wala kope zangu kusinzia,
5 hadi nitakapompatia Bwana mahali,
makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
6 Tulisikia habari hii huko Efrata,
tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara#132:6 yaani Kiriath-Yearimu:
7 “Twendeni kwenye makao yake,
na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
8 inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,
wewe na Sanduku la nguvu zako.
9 Makuhani wako na wavikwe haki,
watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”
10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,
usimkatae mpakwa mafuta wako.
11 Bwana alimwapia Daudi kiapo,
kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:
“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe
kwenye kiti chako cha ufalme,
12 kama wanao watashika agano langu
na sheria ninazowafundisha,
ndipo wana wao watakalia kiti chako cha ufalme
milele na milele.”
13 Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni,
amepaonea shauku pawe maskani yake:
14 “Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;
hapa ndipo nitakapoketi nikitawala,
kwa sababu nimepaonea shauku:
15 Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele:
nitashibisha maskini wake kwa chakula.
16 Nitawavika makuhani wake wokovu,
nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.
17 “Hapa nitamchipushia Daudi pembe#132:17 pembe inawakilisha nguvu,
na kuweka taa kwa ajili ya masiya#132:17 yaani mpakwa mafuta wangu.
18 Adui zake nitawavika aibu,
bali taji kichwani pake litangʼaa sana.”
Selectat acum:
Zaburi 132: NEN
Evidențiere
Copiază
Compară
Împărtășește
Dorești să ai evidențierile salvate pe toate dispozitivele? Înscrie-te sau conectează-te
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.