YouVersion လိုဂို
ရွာရန္ အိုင္ကြန္

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANEနမူနာ

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

7 ၏ ေန႔ 2

  

YESU AMPONYA KIJANA MWENYE PEPO

37 Kesho yake, waliposhuka kutoka mlimani, alikutana na umati mkubwa wa watu.

38 Mtu mmoja katika ule umati wa watu akapiga kelele, akasema,

“Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, ndiye mtoto wangu wa pekee.

39 Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana na hamwachi ila mara chache.

40 Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.

Yesu akajibu akawaambia, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”

Hata yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo mchafu akamwangusha, akamtia kifafa.

Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu amtoke, akamponya yule mtoto, akamrudisha kwa baba yake.

43 Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu.