Kutoka 32:5-6
Kutoka 32:5-6 SWC02
Kisha Haruni akamujengea yule mwana-ngombe mazabahu, halafu akatangaza: Kesho kutakuwa sikukuu kwa ajili ya Yawe. Kesho yake watu wakaamuka mapema wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Watu wakaikaa chini kwa kula na kunywa, kisha wakasimama na kucheza.

