“Heri Yawe angelituua tulipokuwa katika inchi ya Misri ambako tulikaa, tukakula nyama na mikate hata tukashiba. Lakini ninyi mumetuleta huku katika jangwa kwa kuua jamii hii yote kwa njaa!”
Halafu Yawe akamwambia Musa: “Mimi nitawanyeshea mikate kutoka mbinguni. Kila siku watu watatoka na kukusanya chakula cha siku hiyo. Kwa njia hii nitawapima nione kama watafuata sheria zangu au hawatazifuata.