Hekima Ya KirohoEgzanp

Ni lazima tutafute hekima ya kiroho kama vile hazina iliyofichwa (Methali 2:18; Ayubu 28:12 - 28).
Methali 2 inarekodi himizo la Sulemani kwa mwanawe kutafuta hekima kama fedha na kuitafuta kana kwamba ni hazina iliyofichwa (2:4). Mara nyingi tunakosa upambanuzi katika kufanya maamuzi yetu kwa sababu sisi ni wavivu sana hata hatuchukui muda kutafuta upambanuzi kwa kile ambacho Mungu angetaka tufanye. Kwa Sulemani, lengo la kutafuta na kuchimba kwa ajili ya kupata hekima lilikuwa kwamba Bwana hutoa hekima:
Kwa kuwa Bwana huwapa hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu (Methali 2:6).
Kwa maneno mengine, hekima ya kiroho inapatikana tunapotafuta mtazamo wake Mungu (au ujuzi wa Mungu) kwa kujifunza Neno lake. Kisha Roho Mtakatifu anatumia ujuzi huu wa Maandiko kwa hali maalum na maswali tunayokutana nayo tunaposafiri maishani.
Tunapotafuta hekima ya Mungu kwa kujifunza na kukariri Maandiko, tutaona, kama mtunga Zaburi alivyofanya, kwamba Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu (Zaburi 119:105).
“Hazina yako iliyofichwa” unayochimba ni ipi? Je, unatafuta kwa bidii hazina ya kumjua Mungu kupitia Neno Lake na kupata hekima yake ya kiroho kwa ajili ya maisha yako?
Konsènan Plan sa a

Safari zetu katika maisha mara nyingi zinaweza kuhisi kama barabara nyembamba, yenye hila. Hekima ya kiroho ni njia ya Mungu ya kushughulikia safari yetu ya maisha iliyopinda pinda, na isiyonyoofu. Mpango huu wa siku tatu wa Dk. Tony Evans utakuambia hatua za kufikia na kupata hekima hiyo ya kiroho.
More
Plan ki liye yo

Parabòl Jezi : Eksplikasyon pratik sou Peyi Wa a

Mirak Jezi : Revele idantite divin Li

Karèm/Pak : Jezi soufri, mouri, epi genyen viktwa

Ansèyman Jezi : Desizyon saj & benediksyon ki dire

Bondye pa ChatGPT

Karèm/Pak : Jezi fè fas ak lanmò avèk kouraj

Karèm/Pak : Dènye jou Jezi yo

Istwa Nwèl : 5 jou sou nesans Jezi

Grandi Nan Sanktifikasyon
