YouVersion Logo
Search Icon

Hagai UTANGULIZI

UTANGULIZI
Tunavyoambiwa mwanzoni mwa kitabu hiki, Hagai alihubiri kuanzia mwaka wa pili wa utawala wa Dario mfalme wa Persia, yaani katika mwaka wa 520 K.K., karibu miaka 20 baada ya Wayahudi waliokuwa uhamishoni Babuloni kuruhusiwa na mfalme wa Persia kurudi makwao. Kundi la kwanza la Waisraeli lilirejea makwao kuanzia mwaka wa 538 K.K. Baada ya Wayahudi kurejea makwao, walianza shughuli za kujenga upya hekalu lililoharibiwa na Wababuloni katika mwaka wa 587. Lakini walikata tamaa; ndio maana nabii anawatia moyo waendelee. Anawatangazia kwamba, hekalu jipya litapendeza kuliko lile la kwanza (2:1-9) na kwamba ujenzi wake utamaliza hali ya unajisi na umaskini uliowapata watu wa Mungu (2:10-20).
Hagai aliwatia watu moyo kwa maneno yake, yaliyowahimiza watu wa nyakati zake wawe na bidii na kufanya kazi wakitazamia hali mpya ambayo Mungu amewatayarishia.

Currently Selected:

Hagai UTANGULIZI: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy