1
Wakolosai 1:13
Biblia Habari Njema
Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi.
Compare
Explore Wakolosai 1:13
2
Wakolosai 1:16
Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.
Explore Wakolosai 1:16
3
Wakolosai 1:17
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.
Explore Wakolosai 1:17
4
Wakolosai 1:15
Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Explore Wakolosai 1:15
5
Wakolosai 1:9-10
Kwa sababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daima tangu wakati tulipopata habari zenu. Tunamwomba Mungu awajazeni ujuzi kamili wa matakwa yake, pamoja na hekima yote na ujuzi wa kiroho. Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.
Explore Wakolosai 1:9-10
YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy
Home
Bible
Plans
Videos