Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano

Jesus: Our Banner of Victory

SIKU 7 YA 7


Ushindi dhidi ya mauti 


Yesu alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu na kununua msamaha wetu, alituokoa na kutengwa milele na Mungu. Alibadilisha kutukuwa na matumaini dhidi ya mauti na tumaini lililo hai la umilele ujao katika uwepo wa Bwana. Na alipofufuka kutoka kaburini, Yesu alionyesha ushindi wake juu ya mauti, alithibitisha kwamba nguvu ya mauti haina nguvu kilinganisha na ya kwake. Katika Ufunuo1:18, alitangaza "“na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.”


Wakati mauti ni ukweli mgumu kwetu katika maisha haya, tunapowapoteza wapendwa wetu na kuona jinsi mauti ya duniani ilivyo, nakufahamu kweli kwamba Yesu anashikilia funguo za mauti, na amefanya njia kwa ajili yetu kupita katika mlango tofauti kuingia uzima wa milele. Mauti duniani siyo mwisho wa habari. Kuna mengi yajayo! Yesu aliahidi katika Yohana 11: 25, "Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi.”


Kwa sababu Yesu ametuokoa katika mauti ya milele, hatutakiwi kuishi katika hofu. Tuko huru kuishi kwa ujasiri, maisha tele, tukijua kwamba hata iweje hapa duniani, tutaishi milele katika uwepo wa Mungu na katika ushirika wa familia yake. Hata tunapohuzunika kwa wapendwa wetu, tunahuzunika kwa matumaini, tukijua kwamba wakiweka imani yao kwa Yesu, tutaungana nao tena na kufurahia utukufu wa Mungu pamoja.


Katika jumapili hii ya Pasaka, hebu matokeo ya ushindi wa Yesu dhidi ya mauti yazame ndani ya moyo wako na kuhamisha ufahamu wako wa udhaifu wa maisha haya na kujua usalama wa milele mbinguni. Mauti haiumi! Furahia ushindi wake, ujawe na shukurani, na ukue katika uhakika kwamba kila mtu hapa duniani anahitaji tumaini la mbinguni ulilonalo. Hilo ndilo lilikuwa lengo lake la kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu: kwamba hata mmoja wetu asipotee mbali na umilele wake. Hakuna njia bora ya kuonyesha shukrani yako kwa kile alichofanya kwa ajili yako zaidi ya kuuambia ulimwengu juu ya upendo wake kwa ajili yao. Hivyo ndivyo tunavyoishi katika maisha haya. Kwa hiyo utoke na uishi maisha makamilifu- kwa sababu yu hai!


Download today's image here


siku 6

Kuhusu Mpango huu

Jesus: Our Banner of Victory

Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, heb...

More

Tungependa kushukuru Church of the Highlands kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.churchofthehighlands.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha