Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano

Jesus: Our Banner of Victory

SIKU 1 YA 7


Ushindi dhidi ya dhambi


Adamu na Hawa walipomuasi Mungu na kula tunda la mti wa mema na mabaya katika bustani ya Edeni, dhambi ikawa sehemu ya asili ya mwanadamu. Tangu hapo mwanadamu amekuwa akizaliwa akiwa ametengana na Mungu kwa sababu ya dhambi. Kwa sababu yeye ni mkamilifu, Mungu hawezi kuikaribia dhambi. Katika Agano la Kale, wana wa Israeli walitakiwa maramara kutoa sadaka ya kondoo asiyekuwa na mawaa ili kuondoa dhambi. Sadaka ilitakiwa kuwa kamilifu ili kulipa denimla dhambi -ilikuwa ni njia pekee mtu anaweza kupatana na Mungu.


Yesu mara nyingi ametajwa kama " Mwanakondoo wa Mungu", kwa sababu kifo chake msalabani kilifuta dhambi zote za wanadamu. Moja kati ya miujiza mingi ya msalaba ni kwamba ilipindua laana ya dhambi ya Adamu na Hawa: Kama vile tendo moja la dhambi liliwatenganisha wanadamu wote na Mungu, dhabihu iliyotolewa na mtu mmoja mkamilifu iliondoa dhambi za watu wote na kutengeneza njia ya upatanisho. Kwa sababu Yesu alijitoa kwa ajili yetu, tuna nafasi ya kuwa na uhusiano na Mungu tena. Mungu anapotutazama, haoni dhambi zetu- anaona haki ya mwana wake.


Tunapoingia juma hili la Pasaka, chukua muda kutafakazi zawadi kubwa Yesu aliyotupa alipoutoa uhai wake kulipa dhambi zetu. Mtume Paulo katika Warumi 6: 23 anaanza kwa kusema " Mshahara wa dhambi ni mauti." Tulikuwa tumekufa katika Hali ya uovu wetu, tukiwa tumetengwa milele na Mungu. Lakini Paulo anaendelea na mstari na ukweli wa ukombozi: "Lakini karama ya Mungu uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu." Kwa sababu ya Yesu, denimla dhambi limelipwa, na tunakaa milele katika uwepo wa Mungu!


Pia, kwa kuwa Yesu ametufunika na haki yake, tuko huru na nguvu ya dhambi katika maisha yetu. Usiruhusu kujiweka utumwani na tabia zako za zamani za dhambi. Yesu ameishinda dhambi, na ameshiriki nawe ushindi huo bure! Ni kwa uhuru huo nawe umewekwa huru. Tembea katika uhuru huo!.


Download today's image here


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Jesus: Our Banner of Victory

Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, heb...

More

Tungependa kushukuru Church of the Highlands kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.churchofthehighlands.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha