YouVersion 標識
搜索圖示

Mwanzo Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kiliandikwa kuelezea vile vitu vyote vilianza. Neno “Mwanzo” linatokana na maana ya “asili” au “chanzo.” Kinaelezea kwamba Mwenyezi Mungu aliumba ulimwengu wote, vile mwanadamu aliumbwa na kuwekwa katika mazingira yaliyokuwa kamili, vile dhambi ilianza, na vile Mwenyezi Mungu alitoa wokovu kwa mwanadamu aliyepotea. Mwanzo wa historia ya mwanadamu unaelezewa, mwanzo wa sanaa na mwanadamu kutengeneza vifaa, vile lugha za wanadamu zilianza, na kule mataifa tofauti yalitokea. Kitabu kinaendelea kuelezea chanzo cha Waebrania naye Ibrahimu, akifuatiwa na habari za Isaka, Yakobo na wanawe, na kitabu kinaishia na Yusufu akiwa Misri.
Wazo Kuu
Wazo kuu katika kitabu hiki ni kwamba, ingawa Mwenyezi Mungu aliumba vitu vyote vikiwa vizuri nayo dhambi ya mwanadamu ikaviharibu, Mwenyezi Mungu hajakufa moyo, bali sasa anamtafuta mwanadamu ili kumwokoa. Mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu ya mambo yote yanasisitizwa, mtazamo wa kipekee ukiwa vile Mwenyezi Mungu anaendesha historia kuleta wema kwa watu wake na wokovu wao (50:20).
Mwandishi
Musa.
Tarehe
Kama mwaka wa 1420 au 1220 KK.
Mgawanyo
Kuumbwa kwa ulimwengu, na mwanadamu (1:1–2:25)
Kuanguka kwa mwanadamu, na chanzo cha dhambi (3:1–4:26)
Historia ya mwanadamu aliyeanguka hadi gharika (5:1–9:29)
Binadamu kuenea duniani kote (10:1–11:32)
Maisha ya Ibrahimu (12:1–25:18)
Maisha ya Isaka (25:19–26:35)
Maisha ya Yakobo na Esau (27:1–37:1)
Maisha ya Yusufu (37:2–50:26).

目前選定:

Mwanzo Utangulizi: NMM

醒目顯示

分享

複製

None

想要在所有設備上保存你的醒目顯示嗎? 註冊或登入

YouVersion 使用 cookie 來個性化你的體驗。透過使用我們的網站,你即接受我們按照我們的 隱私政策所述來使用 cookie。