1
Mwanzo 15:6
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Abramu akamwamini BWANA, naye kwake jambo hili likahesabiwa kuwa haki.
對照
Mwanzo 15:6 探索
2
Mwanzo 15:1
Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono, akaambiwa: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.”
Mwanzo 15:1 探索
3
Mwanzo 15:5
Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
Mwanzo 15:5 探索
4
Mwanzo 15:4
Ndipo neno la BWANA lilipomjia, likanena: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.”
Mwanzo 15:4 探索
5
Mwanzo 15:13
Kisha BWANA akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni katika nchi isiyo yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.
Mwanzo 15:13 探索
6
Mwanzo 15:2
Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina mtoto, na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?”
Mwanzo 15:2 探索
7
Mwanzo 15:18
Siku hiyo BWANA akafanya agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri hadi mto ule mkubwa, Frati
Mwanzo 15:18 探索
8
Mwanzo 15:16
Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana uovu wa Waamori bado haujafikia kipimo.”
Mwanzo 15:16 探索
主頁
聖經
計劃
影片