Mateo 6:19-21
Mateo 6:19-21 SRB37
Msijilimbikie malimbiko nchini, mende na kutu zinapoyaharibu! Nao wezi huyafukua na kwiba. Lakini jilimbikieni malimbiko mbinguni, yasikoharibiwa na mende wala na kutu, wala wezi wasikoyafukua na kwiba! Kwani limbiko lako liliko, ndiko, nao moyo wako utakakokuwa.