Malaki 4

4
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja
1Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, siku yaja, nayo inawaka kama tanuri. Wenye kiburi na waovu wote watatupwa humo na kuteketea kama mabua makavu; watateketea kabisa pasibaki hata alama. 2Lakini kwa ajili yenu nyinyi mnaonicha, uwezo wangu wa kuokoa utawachomozea kama jua lililo na nguvu za kuponya kwenye mionzi yake. Mtatoka mkirukaruka kama ndama watokapo zizini mwao. 3Siku hiyo mtawakanyagakanyaga waovu, nao watakuwa kama majivu chini ya nyayo zenu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
4“Kumbukeni sheria, kanuni na maagizo yangu niliyomwamuru Mose mtumishi wangu kule mlimani Horebu, ili awaamuru watu wote wa Israeli.
5 # Taz Mat 11:14; 17:10-13; Marko 9:11-13; Luka 1:17; Yoh 1:21 “Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia. 6Nabii Elia atawapatanisha wazazi na watoto wao; la sivyo, nitakuja na kuiangamiza nchi yenu.”

目前选定:

Malaki 4: SCLDC10

高亮显示

分享

复制

None

想要在所有设备上保存你的高亮显示吗? 注册或登录