1
Luka 8:15
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Lakini zilizoko penye mchanga mzuri ndio hao: wanalisikia Neno na kulishika katika mioyo iliyo mizuri na miema; ndio wanaozaa matunda kwa kuvumilia.*
对照
探索 Luka 8:15
2
Luka 8:14
Lakini zilizoangukia miibani ndio hao: wanalisikia, lakini huenda zao, Neno likisongwa nayo masumbuko na mali nyingi na furaha za ulimwenguni; hivyo hawaivishi punje.
探索 Luka 8:14
3
Luka 8:13
Nazo zilizoko mwambani ndio hao: wanapolisikia Neno hulipokea kwa furaha, lakini hawana mizizi, hulitegemea kitambo kidogo, kisha siku za kujaribiwa hujitenga.
探索 Luka 8:13
4
Luka 8:25
Kisha akawaambia: Tegemeo lenu liko wapi? Kwa kuogopa wakastaajabu tu, wakasemezana wao kwa wao: Ni mtu gani huyu, ya kuwa anaagiza hata upepo na maji, nayo yanamtii!
探索 Luka 8:25
5
Luka 8:12
Zilizoko njiani ndio wenye kulisikia; kisha huja Msengenyaji, akaliondoa Neno mioyoni mwao, wasipate kulitegemea na kuokoka.
探索 Luka 8:12
6
Luka 8:17
Kwani hakuna ililofichwa lisiloonekana halafu; wala hakuna njama isiyotambulikana halafu na kutokea waziwazi.
探索 Luka 8:17
7
Luka 8:47-48
Yule mwanamke alipoona, ya kuwa hakufichika, akaja na kutetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu ya kumgusa na jinsi alivyopona papo hapo. Naye akamwambia: Mwanangu, kunitegemea kwako kumekuponya, nenda na kutengemana!
探索 Luka 8:47-48
8
Luka 8:24
Ndipo, walipomjia, wakamwamsha wakisema: Bwana, Bwana, tunaangamia! Naye alipoinuka, akaukaripia upepo na mawimbi ya maji, yakatulia, kukawa kimya.
探索 Luka 8:24
主页
圣经
计划
视频