Kwani mkuyu hauchanui, wala mizabibu haizai,
vichipukizi vya mchekele navyo hudanganya,
mashamba ya ngano hayaleti chakula,
kondoo wametoweka mazizini kwao,
hata ng'ombe hamna vibandani mwao.
Lakini mimi ninayemfurahia, ndiye Bwana,
ninamshangilia Mungu wangu aliyeniokoa.