1
Waamuzi 16:20
BIBLIA KISWAHILI
RSUVDC
Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.
对照
探索 Waamuzi 16:20
2
Waamuzi 16:28
Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, nikumbuke nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
探索 Waamuzi 16:28
3
Waamuzi 16:17
Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
探索 Waamuzi 16:17
4
Waamuzi 16:16
Hatimaye, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumuudhi, roho yake ikataabika karibu kufa.
探索 Waamuzi 16:16
5
Waamuzi 16:30
Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
探索 Waamuzi 16:30
主页
圣经
计划
视频