1
Yoshua 6:2
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Kisha BWANA akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na wapiganaji wake.
对照
探索 Yoshua 6:2
2
Yoshua 6:5
Utakapowasikia wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na wapiganaji watapanda, kila mtu akielekea mbele yake.”
探索 Yoshua 6:5
3
Yoshua 6:3
Zunguka mji mara moja pamoja na watu wote wenye silaha. Fanya hivi kwa siku sita.
探索 Yoshua 6:3
4
Yoshua 6:4
Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo dume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo.
探索 Yoshua 6:4
5
Yoshua 6:1
Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa sababu ya Waisraeli. Hakuna mtu yeyote aliyetoka au kuingia.
探索 Yoshua 6:1
6
Yoshua 6:16
Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipiga baragumu kwa sauti kubwa, naye Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana BWANA amewapa mji huu!
探索 Yoshua 6:16
7
Yoshua 6:17
Mji huu pamoja na vyote vilivyomo utatengewa BWANA kwa ajili ya kuangamizwa. Rahabu yule kahaba atasalimishwa, pamoja na wote walio naye nyumbani mwake, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma.
探索 Yoshua 6:17
主页
圣经
计划
视频