Injili Ulimwenguni - Sehemu 3నమూనా

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3

7 యొక్క 4

Yesu amponya mtu mwenye ukoma

Ikawa siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia.

Alipomwona Yesu, alianguka chini mpaka uso wake ukagusa ardhi na kumsihi akisema

"“Bwana, ukitaka waweza kunitakasa.”

"Yesu akanyosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka, takasika!” 

"Naye mara ukoma ukapona. Yesu akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu ye yote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe dhabihu alizoagiza Mose ili kuwa ushuhuda kwao.”

Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wo wote, makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.

Lakini mara kwa mara Yesu alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba

వాక్యము