Injili Ulimwenguni - Sehemu 2ნიმუში

Kujaribiwa Kwa Yesu
Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kuingia nyikani ili akajaribiwe na ibilisi.
Baada ya kufunga siku arobaini mchana na usiku, hatimaye akaona njaa.
Mjaribu akamjia na kumwambia, “Kama wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”
Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na kumweka juu ya mnara mrefu mwembamba wa Hekalu,akamwambia,
"“Kama wewe ndiye Mwana wa Mungu jitupe chini, kwa kuwa imeandikwa,“ ‘Atakuagizia malaika zake,nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’ ”
Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia,“Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”
Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, nawe utamtumikia yeye peke yake.”
Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumtumikia.
წმიდა წერილი
About this Plan

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.
More
Related Plans

The Inner Life by Andrew Murray

The Intentional Husband: 7 Days to Transform Your Marriage From the Inside Out

The Faith Series

After Your Heart

Eden's Blueprint

Nearness

"Jesus Over Everything," a 5-Day Devotional With Peter Burton

Paul vs. The Galatians

A Heart After God: Living From the Inside Out
