Logo de YouVersion
Ícono Búsqueda

Mattayo MT. 2

2
1ALIPOZALIWA Yesu katika Bethlehemu ya Yahudi zamani za mfalme Herode, majusi wa mashariki walifika Yerusalemi, 2wakinena, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyola yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudu. 3Mfalme Herode aliposikia haya, akafadhaika, na Yerusalemi pia pamoja nae.
4Akakusanya makuhani wakuu wote na waandishi wa watu, akatafuta khabari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda,
Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda:
Kwa kuwa kwako atatoka liwali
Atakaewachunga watu wangu Israeli.
7Kisha Herode akawaita majusi kwa faragha, akapata kwao hakika ya muda ile nyota ilipoonekana.
8Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkahoji sana mambo ya mtoto; mkiisha kumwona, nileteeni khabari, illi nami nije nimsujudie. 9Nao waliposikia maneno ya mfalme wakashika njia; na tazama ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hatta ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10Walipoiona ile nyota, wakafurahi furaha kuliwa mno.
11Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane. 12Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. 13Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake hatta Misri; 15akawa huko mpaka alipokufa Herode: illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwaua wangu.
16Bassi Herode, akiona ya kuwa amedhihakiwa na majusi, akaghadhabika sana, akatuma watu kuwaua watoto wote wanawaume waliokuwa Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wa miaka miwili na waliopungua, kwa muda aliouhakiki kwa majusi. 17Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
18Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio, na kulalama, na maombolezo,
Rahel akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, maana hawako.
19Hatta alipofariki Herode, malaika wa Bwana akamtokea Yusuf katika ndoto huko Misri, akinena, 20Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ushike njia kwenda inchi ya Israeli: kwa maana wamekufa walioilafuta roho ya mtoto.
21Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake, akatika inchi ya Israeli.
22Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya, 23akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.

Actualmente seleccionado:

Mattayo MT. 2: SWZZB1921

Destacar

Compartir

Copiar

None

¿Quieres guardar tus resaltados en todos tus dispositivos? Regístrate o Inicia sesión

YouVersion utiliza cookies para personalizar su experiencia. Al usar nuestro sitio web, acepta nuestro uso de cookies como se describe en nuestra Política de privacidad