Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Utukufu Wa Majina Ya MunguMfano

Utukufu Wa Majina Ya Mungu

SIKU 1 YA 4

Kama Mkristo yeyote mwenye afya njema, unataka kumjua Mungu. Unataka kumjua kiuhakika — sio tu kujua kumhusu yeye. Na kusudi uongeze ukaribu wako naye Mungu, itakuwa umefanya kazi ya kukutana naye kwa njia mbalimbali. Umejifunza Neno lake. Umeomba. Umemwabudu Yeye. Umefanya miunganisho na kujenga uhusiano na watoto wake kama mshiriki wa kanisa. Zote hizi ni shughuli nzuri na zinazosaidia.

Lakini hebu nikuulize swali rahisi: unalijua Jina la Mungu?

Hilo si swali la kudanganya. Kama Wakristo wa kisasa, tuna njia nyingi za kushughulikia Utu wa Kimungu tunayemfikiria kama Mungu. Tunamwelewa kwa kumtaja kulingana na Utatu—Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Tunamtambua kama Muumba wetu. Tunalinena jina la Yesu, na tunamtangaza kuwa ndiye Kristo, Bwana na Mwokozi wetu.

Nyingi ya tuyatajayo ni vyeo ambavyo kwa hakika ni vya Mungu. Hata hivyo, Wakristo wengi leo wana maarifa kidogo mno kuhusu jina la Mungu la kina – Au ni seme, majina yake.

Katika Maandiko, majina mara nyingi huwa ni fafanuzi lenye kusudi, mamlaka, umbile, na sifa. Kwa kweli, katika Biblia mara nyingi majina yalitumiwa karibu kuwa sawa na mtu au kitu. Jina la kitu lilibeba uzito karibia sawa na kama kitu chenyewe. Ndiyo maana Yesu aliposema kwamba amewajulisha jina la Mungu, asema, “Nami nimewajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo…. (Yoh. 17:26). Alikuwa anazungumzia zaidi ya sauti zilizowekwa pamoja katika neno moja. Yesu, akiwa amekuja duniani katika mwili, alifunua moyo wake Mungu, akili, mapenzi, sifa, na kuwa kwake—yote kupitia kwa ufunuo wa Jina Lake.

Kwa sababu ya kina cha sifa ya Mungu, yeye analo jina la kuakisi sifa na uwezo wake tofauti tofauti na jinsi anavyohusiana na wanadamu. Anayo majina mengi na haya baadhi ya machache tu:

  • Elohimu
  • Yehova
  • El Elyoni
  • El Shadai
  • Adonai
  • Immanueli
  • Na mengine mengi.

Ninachotaka uelewe ni kwamba Mungu analo jina la hali yoyote na kwa kila hali ambayo unaweza kujikuta humo. Nakutia moyo upate kuyajua majina ya Mungu, maana ni katika kuijua sifa yake na uwezo wake ndipo utajifunza kupumzika na kugundua amani na nguvu katika utunzaji wake wa kiagano.

Kwa maneno mengine, jifunze Majina ya Mungu ili uweze kumjua kweli.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Utukufu Wa Majina Ya Mungu

Mungu ana majina kadha wa kadha ambayo yanamwelezea katika Maandiko. Kila jina hutuambia sifa na moyo wake kwa njia ya kina na kibinafsi. Katika mpango huu wa kusoma na Tonay Evans, fichua ukuu wa majina ya Mungu.

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha