Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo MajonziMfano

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

SIKU 1 YA 7

Kupona kutoka kwa Hasara

Yesu alilia kwa huzuni kutokana na kifo cha rafiki yake Lazaro. Alifahamu vyema huzuni ni nini. Mungu anaelewa hasara au huzuni yoyote iwezayo kutukumba. Kwa kweli, Roho Mtakatifu pia anaitwa Mfariji. Hakika mojawapo ya faraja zake ni amani tunapohuzunika kwa majonzi ya kina. Hasara gani imekuletea huzuni? Ichukue kwa Bwana. Usiruhusu majonzi uliyo nayo ifanyike kuwa chanzo cha uchungu unatoa nafasi kwa adui.

Mungu anatamani uhusiano wa kina na wa kudumu na wewe. Kwa sababu Yeye ni wa kutegemewa, anakutaka umtegemee. Mungu anaweza kutumia huzuni yako kuimarisha uhusiano wako naye.

Ikiwa wewe ni mzima wa afya, uwezekano wako haupo wa wewe kwenda kwa ofisi ya daktari wakati wowote hivi karibuni. Hii ni kwa sababu katika mwili wako kila kitu kinaonekana kufanya kazi na kufanya kile kinachopaswa kufanya. Lakini wakati unapokuwa mgonjwa, na hasa ikiwa ugonjwa huo utaendelea kwa muda mrefu, kuna uwezekano kwamba utafanya mpango wa kwenda kumwona daktari wako. Utachagua kuingia uweponi mwa daktari wako.

Vivyo hivyo, wakati mwingine Mungu huruhusu hasara katika maisha yako ili akurudishe umakini wako umwelekee yeye. Hakutaki utembee pekee yako kwenye hii barabara. Yuko pamoja nawe hata unaposahau kwamba yupo. Anatamani kuwa karibu na wewe.

Je, uko katika hali ambayo inataka kula ukiwa hai? Je, unajikuta ukiwa na matumaini machache siku baada ya siku? Je, umewahi jihisi kuwa umeshindwa kabisa na kujutia kile ulichopoteza?

Ikiwa hiyo inaelezea hali yako, basi sitaki chochote zaidi ya kukukumbusha kwamba Yesu yuko pamoja nawe. Yupo pamoja nawe sasa hivi. Na ninataka ujue kikamilifu kwamba, kwa sababu yuko pamoja nawe, nguvu zake na neema yake iko pamoja nawe. Na nguvu zake na neema zake zitakufariji.

Wakati fulani Mungu anatuita tutembee kupitia kwenye bonde. Siwezi kuahidi kwamba maisha hayatakuwa na upepo, mawingu, na mvua. Lakini ninaweza kuahidi kwamba huna budi kupita kwenye bonde la hasara peke yako. Ukiyatupa macho yako kwake Yesu Kristo, atakutana nawe hapo ulipo. Kwa hivyo endelea kutembea. Usikate tamaa. Usiseme kwamba huwezi kufanikiwa, kwa sababu Mungu atafanya pamoja nawe. Hutembei barabara hii peke yako.

Hebu tuombe:

Bwana, Wewe ndiwe Muumba wa vitu vyote. Kwa kweli, Unashikilia vitu vyote mkononi Mwako. Hakuna kitu chochote ambacho nimepoteza maishani mwangu kilitokea kwa mshangao kwako. Unayajua yote na kwa ukuu wako umeyaruhusu yote. Nisaidie kurejesha imani na matumaini yangu pale ambapo imevunjwa. Nipe moyo unaotamani mapenzi yako maishani mwangu. Na tafadhali nisaidie nigeuze mawazo yangu kutoka kwa yale niliyopoteza na kuzingatia ahadi nilizo nazo ndani yako – huku mojawapo ya ahadi hizo ikiwa ni kwamba hutaniacha kamwe wala kunipungukia. Katika jina la Kristo, amina.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

Siku 7 za Sala zimeundwa kwa minajili ya kuimarisha roho yako na kuhimiza moyo wako wakati upitiapo majonzi. Kila siku inajumuisha sala utakayofanya wewe au kutumia kama msingi wa maombi yako kuhusu mada ya siku hiyo ili...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha