Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

SIKU 2 YA 6

Dirii ya haki

“Mungu ameunda ndoa kwa madhumuni yaliyowekwa na Mungu ya kutumia mamlaka juu ya nyanja ya ulimwengu wako ambapo una wajibu na ushawishi. Kama wanandoa, mnapaswa kuwashawishi wale wanaowazunguka badala ya kushawishiwa na ulimwengu.” Tony Evans

Baba, unatuambia kwamba tunapokufuata wewe na Neno lako, nia zetu zitabadilishwa na kufanywa upya. Kisha tutakuwa katika nafasi ya kutambua ni nini mapenzi yako ya haki kwetu. Lakini tunapopuuza uwepo wako na Neno lako, ni rahisi kufuatisha namna ya udhalimu wa ulimwengu huu. Mungu, tuwezeshe kama wanandoa kukutafuta wewe kila siku, iwe ni katika mazungumzo yetu sisi kwa sisi, wakati tunaposali pamoja, ujumbe mfupi tunazotumiana—kwa njia zozote zile zinazo hesabika — ebu tuwe ukumbusho kwa mmoja kwa mingine kufanya upya nia zetu kwa Neno lako.

Tunajua kwamba wakati nia zetu zinapopatana na yako, udhalimu wa ulimwengu huu utadhihirika. Nasi tutatafuta kuishi kwa kiwango chako, na sio cha ulimwengu. Tuongoze katika kusudi lako kila dakika ya kila siku. Katika jina la Kristo, amina

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia ki...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha