Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 139

139
Mungu Asiyeweza Kukwepwa
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Zaburi.
1 # Yer 12:3; Ufu 2:23 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.
2 # 2 Fal 19:27; Mt 9:4; Yn 2:24 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
4 # Ebr 4:13 Maana hamna neno ulimini mwangu
Usilolijua kabisa, BWANA.
5Umenizingira nyuma na mbele,
Ukaniwekea mkono wako.
6Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,
Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
7Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
8 # Mit 15:11 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika.
11Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,
Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12Giza nalo halikufichi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana;
Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.
Matendo yako ni ya ajabu,
Na nafsi yangu yajua sana,
15Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri,
Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
16Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;
Chuoni mwako ziliandikwa zote pia,
Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu;
Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
18Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga;
Niamkapo nikali pamoja nawe.
19 # Isa 11:4 Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu!
Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu;
20 # Ayu 21:14,15; Yud 1:15 Kwa maana wakuasi kwa ubaya,
Adui zako wakutaja jina lako bure.
21Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia?
Nisikirihike nao wakuasio?
22Nawachukia kwa ukomo wa chuki,
Wamekuwa adui kwangu.
23 # Ayu 31:6 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,
Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24 # Mt 7:14; Yn 14:6 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu,
Ukaniongoze katika njia ya milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 139: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha