YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Upendo Wa BureSample

Upendo Wa Bure

DAY 5 OF 5

Kutoka Maisha ya Unyonge hadi Wakati wa Kurudisha Fahamu Luka 15: 17 inatueleza, “Hatimaye akili zikamrudia” Ni jambo la umuhimu sana, kwa watu wote, kufikia wakati huu. Wakati wa kuona wazi. Wakati wa kutambua wazi na kuwaza “Ngoja kidogo. Ni nini ninachofanya hapa? Nimekuwa nani? Mbona ninaishi hivi? Lazima kuwe na mtindo wa kuridhisha, mtindo mwema katika maisha!” Wengi wenu wanahitaji kurudisha fahamu kama Mwana Mpotevu! Labda ulikuwa katika kanisa au aulikuwa mfuasi wake Yesu mbeleni? Unatakiwa kufahamu kwamba sababu zako duni za kusonga kando na imani yako na kufuatilia mambo ya dunia – hazileti shangwe au nafaka yoyote. Yeremia 2:5 inatupatia onyo, “Bwana asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?” Dunia ilikudanganya na ulikubali uwongo huu! Dunia ilikuahidi utulivu, furaha, kutosheka na kuridhika katika maisha jinsi ulivyotaka katika roho yako, lakini ikakuwacha bila nafsi. Ni wakati wa kurudi nyumbani! Labda haujawahi kuyasikia maneno haya. Labda haukujua kunasuluhisho la maisha ya huzuni na changamoto unayoishi sasa. Labda haukujua kwamba Mungu anayo tiba ya dhambi, magonjwa, kutegemea pombe au madawa ya kulevya na giza zinazojaribu kukumaliza. This is your wake up call – Ni wakati wa kuridi nyumbani! Na Mwana Mpotevu alifanya vivi hivi. Aliamua kunyenyekea, kumridia Baba yake na kujipatia kwake kama mfanyi-kazi wake (kwani wafanyikazi waliishi maisha bora).

Scripture

Day 4

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy