Soma Biblia Kila Siku 04/2020预览

Kitabu cha Zaburi kinamalizika kwa nyimbo sita za sifa za kawaida. Kuna ujumbe mmoja mkubwa katika nyimbo hizi: Mungu ni mkuu mwenye enzi zote, na anastahili kusifiwa na wanadamu, siku hata siku, milele na milele. Lakini juu ya yote, mwanzo na mwisho sifa yake ni: Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma. Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema (m.8). Mungu wetu amejaa wema. Huonyesha uaminifu wa Agano lake kwa watu wake mwenyewe. Na huonyesha neema na upendo wake kwa watu wote wa kila mahali.