Soma Biblia Kila Siku 04/2020预览

Matendo yote ya dhihaka aliyotendewa Yesu katika kuuawa kwake yalikuwa kinyume na jinsi Yesu alivyo katika uhalisi wake. Walifanya yote kwa kumsuta, lakini Yeye atajaonekana katika enzi yake kuu kama Mhukumu mwenye haki, Mfalme na Mtawala. Walimchanganya na wahalifu, lakini kumbe Yeye ni Mtakatifu na tutamwona katika utukufu wa utakatifu wake. Walimshutumu kama asiyeweza kujiokoa kumbe alifufuka kwa uweza akawa mshindi wa mwiba wa mauti na udhalimu wote. Kwake kila goti litapigwa.