Yoshua 12
12
Orodha ya wafalme walioshindwa
1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kumiliki maeneo yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni hadi Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki mwa Araba:
2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi#12:3 yaani Bahari ya Galilaya hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi#12:3 yaani Bahari Mfu), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya miteremko ya Pisga.
4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6Musa, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7Hawa ndio wafalme ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao. 8Nchi hizi ni: nchi ya vilima, Shefela#12:8 au upande wa magharibi chini ya vilima, Araba, miteremko ya milima, jangwa, na Negebu; yaani nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
Wafalme hawa walikuwa:
9mfalme wa Yeriko;
mfalme wa Ai (karibu na Betheli);
10mfalme wa Yerusalemu;
mfalme wa Hebroni;
11mfalme wa Yarmuthi;
mfalme wa Lakishi;
12mfalme wa Egloni;
mfalme wa Gezeri;
13mfalme wa Debiri;
mfalme wa Gederi;
14mfalme wa Horma;
mfalme wa Aradi;
15mfalme wa Libna;
mfalme wa Adulamu;
16mfalme wa Makeda;
mfalme wa Betheli;
17mfalme wa Tapua;
mfalme wa Heferi;
18mfalme wa Afeki;
mfalme wa Lasharoni;
19mfalme wa Madoni;
mfalme wa Hazori;
20mfalme wa Shimron-Meroni;
mfalme wa Akshafu;
21mfalme wa Taanaki;
mfalme wa Megido;
22mfalme wa Kedeshi;
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli;
23mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori);
mfalme wa Goimu katika Gilgali;
24mfalme wa Tirsa;
jumla ya wafalme thelathini na mmoja (31).
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.