1
Waroma 4:20-21
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Hata kile kiagio cha Mungu hakupotelewa nacho, kwani kukitegemea hakukumshinda, ila akakaza kukitegemea kwa nguvu, akamtukuza Mungu. Maana aliyashika moyoni, aliyoyatambua ya kuwa: Yeye ana nguvu ya kuyatimiza, aliyoyaagia.
సరిపోల్చండి
Waroma 4:20-21 ని అన్వేషించండి
2
Waroma 4:17
kama ilivyoandikwa: Nimekuweka, uwe baba yao mataifa mengi. Ni kwa sababu alimtegemea Mungu anayewarudisha wafu uzimani, anayeviita visivyokuwapo, vikapata kuwapo.
Waroma 4:17 ని అన్వేషించండి
3
Waroma 4:25
aliyetolewa kwa ajili ya maanguko yetu, akafufuliwa kwa ajili ya wongufu wetu.
Waroma 4:25 ని అన్వేషించండి
4
Waroma 4:18
Napo hapo palipokuwa pasipo kingojeo cho chote, alifuliza kukitegemea kingojeo cha kwamba: Atakuwa baba ya mataifa mengi, kama ilivyosemwa: Hivyo ndivyo, wao wa uzao wako watakavyokuwa.
Waroma 4:18 ని అన్వేషించండి
5
Waroma 4:16
Kwa hiyo wenye kumtegemea Mungu ndio watakaogawiwa; tena hivyo kile kiagio kinawatimilia wao wote walio uzao wake, sio wenye kuyafuata Maonyo tu, ila nao wenye kuifuata njia yake Aburahamu ya kumtegemea Mungu; hivyo ndivyo, anavyokuwa baba yetu sisi sote
Waroma 4:16 ని అన్వేషించండి
6
Waroma 4:7-8
Akasema: Wenye shangwe ndio walioondolewa mapotovu nao waliofunikwa makosa. Mwenye shangwe ni mtu, Bwana asiyemhesabia makosa.
Waroma 4:7-8 ని అన్వేషించండి
7
Waroma 4:3
Kwani Maandiko yanasemaje? Aburahamu alimtegemea Mungu, kwa hiyo aliwaziwa kuwa mwenye wongofu.
Waroma 4:3 ని అన్వేషించండి