Soma Biblia Kila Siku 04/2026Mfano

“Ikiwa watu wangu … watajinyenyekesha, ... nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao” (2 Nya 7:14*).Unyenyekevu huu hujitokeza kama kupenda maagizo ya Mungu na kutenda fadhili, huruma na haki kama yeye. Mnyenyekevu anaelezewa kamaapendezwaye sana na maagizo yakeMungu (m.1b). Tafakari pia m.4-5:Nuru huwazukia wenye adili gizani; ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki.Watu wakiitikia matendo ya Mungu kwa njia hii, anawabariki kwa kuwapa uzao bora, anawaangalia na kuwahifadhi, hata wasiwe na la kuwahofisha. Uradhi na maisha ya ufadhili namna hii ni tofauti kabisa na wivu na hali ya kukata tamaa ya watu waovu.
* Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV)
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Aprili. Utasoma kitabu cha Zaburi, Yohana, Luka na Isaya. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz




