Soma Biblia Kila Siku 1 - 2026Mfano

Upo msemo wa Kiswahili usemao, “Leo ni leo, asemaye kesho ni muongo”. Mungu hutoa zawadi ya kuishi tukiamka kitandani na kuona siku nyingine mpya imeanza. Kila siku anatutayarishia matendo mema tuyatende. Usingoje kesho, hujui itakuwaje kwako. Hali kadhalika tusipange siku zijazo kana kwamba tunaweza kuziamua sisi wenyewe, bali tujitoe kwa mapenzi ya Mungu, tukimwomba atulinde dhidi ya kiburi, na atupe neema, nia na ujasiri wa kuyatenda. Huu ndio uzima wetu tulio nao kila siku katika Yesu.
* Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV)
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Januari. Utasoma kitabu cha Marko na Ezra. Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz




