Soma Biblia Kila SikuMfano

Katika Injili ya Yohana, “Neno” lilitumika kuhusu mwenye nafsi, yaani Yesu. Hata hapa katika barua ya Yohana, tunakuta matumizi hayo hayo. Mtume anasema walilisikia, waliliona, na kuligusa Neno:Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima ... hilo tuliloliona na kulisika, twawahubiri na ninyi, ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo(m.1, 3*). Hii inamaanisha vyote viwili, ujumbe na Yesu Kristo. Ujumbe ni “Neno la uzima”. Wapokeaji wa barua wanahubiriwa ili wao pia wapate ushirika na Mungu. Huo wapatikana pale ambapo dhambi imeondolewa. Yesu anawapa uzima wale wanaousikia ujumbe wake, kuukubali na kumwamini. Je, wewe ni miongoni mwa hao?
* Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV)
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Karibu katika mpango huu wa Soma Biblia Kila Siku mwezi wa Desemba. Utasoma kitabu cha 1 Yohana . Utapata pia maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa na kutafakari Neno ulilosoma. Isipokuwa imeandikwa vinginevyo, nukuu zote za Biblia katika mpango huu zimechukuliwa kutoka katika Swahili Union Version (SUV).
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

