Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:81-82 - Linganisha Matoleo Yote

Zaburi 119:81-82 BHN (Biblia Habari Njema)

Niko hoi kwa kukungojea uniokoe; naweka tumaini langu katika neno lako. Macho yangu yanafifia nikingojea ulichoahidi. Nauliza: “Utakuja lini kunifariji?”

Shirikisha
Zaburi 119 BHN

Zaburi 119:81-82 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelingojea neno lako. Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako, Nisemapo, Lini utakaponifariji?

Shirikisha
Zaburi 119 SUV

Zaburi 119:81-82 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelitumainia neno lako. Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako, Nikisema, Lini utakaponifariji?

Shirikisha
Zaburi 119 SRUV

Zaburi 119:81-82 NEN (Neno)

Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifariji lini?”

Shirikisha
Zaburi 119 NEN