Zaburi 119:75-77
Zaburi 119:75-77 Biblia Habari Njema (BHN)
Najua hukumu zako ni adili, ee Mwenyezi-Mungu, na kwamba umeniadhibu kwani wewe ni mwaminifu. Fadhili zako na zinipe faraja, kama ulivyoniahidi mimi mtumishi wako. Unionee huruma nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha yangu.
Zaburi 119:75-77 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa. Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu, Kulingana na ahadi yako kwa mtumishi wako. Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.
Zaburi 119:75-77 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa. Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu, Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.
Zaburi 119:75-77 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu. Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.