Zaburi 105:42-45
Zaburi 105:42-45 Biblia Habari Njema (BHN)
Aliikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. Basi akawatoa watu wake nchini, wateule wake wakaimba na kushangilia. Aliwapa nchi za mataifa mengine na kuwakabidhi mashamba ya wenyeji; kusudi watu wake watii masharti yake, na kufuata sheria zake. Asifiwe Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 105:42-45 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Abrahamu, mtumishi wake. Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.
Zaburi 105:42-45 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake. Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.
Zaburi 105:42-45 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe, akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali ambayo wengine walikuwa wameitaabikia: alifanya haya ili wayashike mausia yake na kuzitii sheria zake.