Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 4:10-11 - Compare All Versions

Wafilipi 4:10-11 BHN (Biblia Habari Njema)

Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo. Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitaji kitu; maana nimejifunza kuridhika na vitu nilivyo navyo.

Shirikisha
Wafilipi 4 BHN

Wafilipi 4:10-11 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.

Shirikisha
Wafilipi 4 SUV

Wafilipi 4:10-11 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Nilifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo.

Shirikisha
Wafilipi 4 SRUV

Wafilipi 4:10-11 NEN (Neno)

Nina furaha kubwa katika Bwana kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo. Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote.

Shirikisha
Wafilipi 4 NEN