Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Walawi 7:25-27 - Linganisha Matoleo Yote

Walawi 7:25-27 BHN (Biblia Habari Njema)

Mtu yeyote akila mafuta ya mnyama aliyetolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atatengwa na watu wake. Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.”

Shirikisha
Walawi 7 BHN

Walawi 7:25-27 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. Tena msiile damu yo yote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Mtu ye yote alaye damu, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

Shirikisha
Walawi 7 SUV

Walawi 7:25-27 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Mtu yeyote alaye damu, mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.

Shirikisha
Walawi 7 SRUV

Walawi 7:25-27 NEN (Neno)

Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa BWANA kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. Popote mtakapoishi, kamwe msile damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. Mtu yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Shirikisha
Walawi 7 NEN