Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 51:54-55 - Linganisha Matoleo Yote

Yeremia 51:54-55 BHN (Biblia Habari Njema)

“Sikiliza! Kilio kinasikika kutoka Babuloni! Kishindo cha maangamizi makubwa kutoka nchi ya Wakaldayo! Maana mimi Mwenyezi-Mungu naiangamiza Babuloni, na kuikomesha kelele yake kubwa. Adui ananguruma kama mawimbi ya maji mengi, sauti ya kishindo chao inaongezeka.

Shirikisha
Yeremia 51 BHN

Yeremia 51:54-55 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Sauti ya kilio kutoka Babeli, Na ya uangamivu mkuu toka nchi ya Wakaldayo! Maana BWANA amwangamiza Babeli, Na kuikomesha sauti kuu ndani yake; Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi, Mshindo wa sauti zao wafanya makelele

Shirikisha
Yeremia 51 SUV

Yeremia 51:54-55 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Sauti ya kilio kutoka Babeli, Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo! Maana BWANA amwangamiza Babeli, Na kuikomesha sauti kuu ndani yake; Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi, Mshindo wa sauti zao wafanya makelele

Shirikisha
Yeremia 51 SRUV

Yeremia 51:54-55 NEN (Neno)

“Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli, sauti ya uharibifu mkuu kutoka nchi ya Wakaldayo. BWANA ataiangamiza Babeli, atanyamazisha makelele ya kishindo chake. Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu, ngurumo ya sauti zao itavuma.

Shirikisha
Yeremia 51 NEN