Yeremia 5:3 - Linganisha Matoleo Yote
Yeremia 5:3 BHN (Biblia Habari Njema)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa. Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Yeremia 5:3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Yeremia 5:3 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Yeremia 5:3 NEN (Neno)
Ee BWANA, je, macho yako hayaitafuti kweli? Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo. Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe nao walikataa kutubu.