Yeremia 5:16-17
Yeremia 5:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mishale yao husambaza kifo; wote ni mashujaa wa vita. Watayala mazao yenu na chakula chenu; watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe; wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu. Miji yenu ya ngome mnayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.
Yeremia 5:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia. Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Yeremia 5:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia. Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng’ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Yeremia 5:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Podo zao ni kama kaburi lililo wazi, wote ni mashujaa hodari wa vita. Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, wataangamiza wana wenu na mabinti zenu; wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe, wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. Kwa upanga wataangamiza miji yenye maboma mliyoitumainia.