Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 4:4-6 - Linganisha Matoleo Yote

Waebrania 4:4-6 BHN (Biblia Habari Njema)

Maana Maandiko yasema mahali fulani kuhusu siku ya saba: “Mungu alipumzika siku ya saba, akaacha kazi zake zote.” Tena jambo hili lasemwa pia: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko.” Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii.

Shirikisha
Waebrania 4 BHN

Waebrania 4:4-6 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao

Shirikisha
Waebrania 4 SUV

Waebrania 4:4-6 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na tena kunena hapa napo, Hawataingia pumzikoni mwangu. Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao

Waebrania 4:4-6 NEN (Neno)

Kwa maana mahali fulani amezungumza kuhusu siku ya saba, akisema: “Katika siku ya saba Mungu alipumzika kutoka kazi zake zote.” Tena hapo awali amesema, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.” Kwa hiyo inabaki kuwa wazi kwa wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii.

Shirikisha
Waebrania 4 NEN